Picha

Justin Bieber na Rihanna waahirisha show zao kutokana na maradhi

Rihanna amelazimika kuahirisha show yake ya jijini Boston jana usiku kutokana na kupoteza sauti yake kulikotokana na ugonjwa wa Laryngitis. Show hiyo ipo kwenye ziara yake ya dunia ya Diamonds.

Rihanna-SNL-rihanna-32730715-1600-1200

Kutokana na hatua hiyo,Rihanna alitweet kuwaomba radhi mashabiki wake:

“BOSTON this is the hardest thing for me to deal with! I feel like we’ve been waiting on this day forever, and I’m hurt that I let you down.”

“I hate disappointing people that never ever let me down!! I’m so embarrassed about this! Thank you for your prayers and well wishes! #DWT.” Nayo label yake ya LiveNation, ambayo italazimika kupanga tarehe nyingine ya show hiyo ilitoa maelezo yasemayo:

“Unfortunately, following her sold-out concert on Friday, Rihanna has contracted laryngitis and per doctor’s instruction is unable to perform this evening.”

Naye Justin Bieber ameahirisha show zake mbili zilizokuwa zimepangwa kufanyika wiki hii nchini Ureno kutokana na sababu ambazo hakuzitegemewa.

Picha ya Justin aliyoitweet akiwa hospitali
Picha ya Justin aliyoitweet akiwa hospitali

Bieber alikuwa amepanga kutumbuiza kwenye eneo la Pavilhao Atlantico jijini Lisbon leo March 11 na kesho March 12.
Wiki iliyopita Justin alilazwa nchini Uingereza baada ya kuanguka jukwaani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents