Juventus wamtimbia, Cristiano Ronaldo kwa ‘helicopter’ hotelini

Klabu ya Juventus imekamilisha makubaliano na Real Madrid juu ya kumsajili mchezaji wake, Cristiano Ronaldo na katika kudhihirisha hilo Mwenyekiti wa timu hiyo ya Italia, Andrea Agnelli amekwea ‘helicopter’ kwenda kwenye hoteli ambayo mshambualiaji huyo ametulia na familia yake kukamilisha taratibu zilizo salia.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Skysports kimeripoti kuwa Juventus imeridhia kutoa kitita cha fedha pauni milioni 88 ili kuingia kandarasi na Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa Ballon d’Or akitokea Real Madrid.

Hii leo siku ya Jumatano wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes na Real Madrid wanatarajiwa kumalizana ili mchezaji huyo kutua Juve muda wowote kuanzia sasa.

Ronaldo ametumia misimu tisa Madrid baada ya uhamisho wake wa pauni milioni 80 akitokea Manchester United huku akiondoka na kuwacha rekodi ndani ya klabu hiyo kwa kufunga jumla ya mabao 451.

Nahodha huyo wa Ureno anaondoka Real baada ya kushinda mataji mawili ya La Liga titles, mawili Copa del Rey na mataji manne ya klabu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW