Burudani

Kala Jeremiah kuachia single mpya wiki ijayo ‘JARIBU KUJIULIZA’

JARIBU KUJIULIZA ni jina la single mpya ya Kala Jeremiah kutoka jiji la Miamba Mwanza inayotegemewa kutoa Jumatano wiki ijayo (August 14).

kala

Katika wimbo huo ambao umepikwa na mtayarishaji Nahreel wa Hometown Records, Kala ameunganisha ukomavu wake wa tungo na sauti ya msanii wa kike Mary Lucoss ambaye pia ni zao la shamba la Madam Ritha (BSS).

Kwanini Mary Lucos na siyo msanii mwingine wa kike? Hata Kala mwenyewe ‘alijaribu kujiuliza’ ni msichana gani anayeweza kufit vizuri katika wimbo huu, wazo la mwanzo Kala alihitaji kupata sauti ambayo haijazoeleka sana na baada ya mchakato bahati ilimdondokea Mary atakayesikika katika kiitikio cha wimbo huo.

Wimbo huu utaanza kutoka audio na baadaye video itafuata.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents