Habari

Kampuni ya Apple kuingiza sokoni iPhone 5S yenye ‘finger print sensor’ (September) mwaka huu

Baada ya kampuni ya Apple kupata ushindani kutoka kwa Samsung sokoni siku za hivi karibuni, sasa kampuni hiyo inatarajia kupeleka sokoni toleo jipya la iPhone 5S mwezi (September) mwaka huu.

iphone-plus-blanc-02

Taarifa kutoka katika vyanzo vya kuaminika kwa mujibu wa mtandao wa Ujerumani German blog iFun, iPhone 5S inategemewa kuingia sokoni (September 6) hivyo kuna uwezekano taarifa rasmi ikatoka mwishoni mwa (Agosti) kama ilivyoripotiwa na Daily Mail.

Kwa mujibu wa vyanzo inasemekana toleo jipya la iPhone 5S itakuwa na internet yenye kasi mara kumi ya ile ya 3G. Pia itakuwa na ‘built-in fingerprint scanner’.

iPhone finger

iPhone 5S itakuwa na muonekano wa kufanana na iPhone 5 ya sasa lakini itakuwa na processor yenye speed pamoja na camera iliyoboreshwa zaidi na itakuwa ikitumia iOS 7 software ya Apple iliyozinduliwa mwezi (June)

Kampuni ya Apple imekuwa ikitoa simu mpya kila mwaka toka watambulishe iPhone ya kwanza mwaka 2007. Model za iPhone zilizoishatoka mpaka sasa ni pamoja na iPhone, iPhone 3G, iPhone 3GS na iPhone 4. Model za hivi karibuni ni iPhone 4S na iPhone 5 ambazo zilitambulishwa sokoni (October 2011) pamoja na (September 2012).

Uvumi kuhusu toleo jipya la iPhone5S zilianza kuenea (April) mwaka huu baada ya vyanzo vilivyo karibu na kampuni ya Apple wakiwemo watengenezaji wa simu hizo kuvujisha taarifa kuwa tayari uzalishaji umeanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents