Habari

Kauli ya Rais Magufuli ‘Vijana waachwe walime mpaka kwenye mito’ yazua gumzo bungeni

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Kangi Lugola amesema kuwa hakuna mwananchi anayeruhusiwa kulima kwenye vyanzo vya maji kufuatia kuwa na mkanganyiko wa kauli aliyoitoa jana Rais Magufuli mkoani Kagera ambapo alitokea kijana mmoja alimueleza kuwa alifyekewa mazao yake aliyolima kando ya mto Mkenge, Kyaka mkoani humo ambapo Rais alimruhusu kijana huyo kuendelea kulima eneo hilo.

Mh. Lugola ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma wakati akisisitiza jambo kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji huku akieleza vyanzo vya maji ndivyo uhai wetu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti wapo Watanzania pamoja na vyombo vya habari wameanza kupotosha kauli ya Mh. Rais aliyoitoa jana kule Kagera, kwamba wananchi ni ruksa kwenda kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji, niwahakikishie kauli ya Rais isije ikapotoshwa wananchi wakaenda wakavamia maeneo ya mito na kuanza kulima, na kauli aliyoitoa Mh. Rais Watanzania waelewe vyanzo vya maji ndivyo uhai wetu,” amesema Lugola.

“Watu waelewe mito yote itakauka. Hakuna aneruhusiwa kulima kwenye vyanzo vya maji na hata hivyo Mwenyekiti lakini kwa mujibu wa sheria ya mazingira Mh. Rais ametumia kifungu namba 57 cha sheria hiyo pale ambapo kuna changamoto, wananchi wale waliopo Karagwe pale hawana ardhi Rais ametuomba tushirikiane na uongozi wa mkoa kuhakikisha wale wananchi wanapatiwa maeneo mengine lakini sio kuwaondoa kwahiyo hamruhusiwi na msije kusema Rais amewazuia wananchi kinyume na sheria.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents