Burudani

Kazi aliyonipa Diamond nimeifanya – Q Chief

Msanii mkongwe wa muziki, Q Chief amesema amekamilisha ujio wa wimbo wake mpya wenye mahadhi ya Zouk.

Muimbaji huyo amedai alishauriwa na Diamond Platnumz kufanya muziki wa Zouk kwa kuwa ni muziki ambao alikuwa anaufanya katika kipindi cha nyuma na kumpatia mafanikio makubwa.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Q Chief amedai wimbo huo ambao umetayarishwa na maproducer watatu, utawarudisha nyuma wale mashabiki ambao waliumiss muziki huo.

“Namshukuru Mungu kazi imekamilika na mara ya mwisho kuzungumza na Diamond, aliniambia kwamba anamtaka yule Q Chief wa zamani, yule ambaye alikuwa anaimba Zouk,” alisema Q Chief. “Kazi imekamilika bado maproducer kumalizia kazi zao. Diamond aliniambia nifanye Zouk na kweli nimefanya,”

Q-chief amesema kuwa, ilikua amshirikishe Diamond lakini baada ya watu wake wa karibu kuusikiliza, walimshauri autoe akiwa mwenyewe.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya maandalizi ya show yake ya ‘Miaka 15 ya Qchief’ itayofanyika April 30 katika ukumbi wa Next Door, Masaki, jijini Dar es salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents