Habari

Kelly Rowland atumbuiza kwenye ‘private party’ katika jumba la kifahari la bilionea wa Afrika Kusini

Haijalishi iwe ni Kipaimara, vigodoro au birthday, kama mkwanja upo basi unaweza kumleta staa yeyote kutumbuiza. Baada ya rapper Kanye West kutumbuiza katika harusi ya mjukuu wa Rais wa Kazakhstan hivi karibuni, staa mwingine wa Marekani Kelly Rowland atumbuiza katika jumba la bilionea wa Afrika.

LOS ANGELES, CA - FEBRUARY 10: Singer Kelly Rowland arrives at the 55th Annual GRAMMY Awards at Staples Center on February 10, 2013 in Los Angeles, California.   Jason Merritt/Getty Images/AFP

Mwimbaji wa R&B na member wa zamani wa kundi la Destiny’s Child mwishoni mwa mwezi uliopita (September) alikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kutumbuiza katika ‘private party’ kwenye jumba la kifahari ‘mansion’ la Bilionea Douw Steyn.

steynnnnn mansion
Hii ndio mansion ya Steyn iliyoko Afrika Kusini ambapo Kelly alienda kutumbuiza

Rowland aliwasili nchini humo Sept 25 kwaajili ya kupamba ‘private party’ ya siku mbili Sept 27 na 29 mwaka huu katika jumba hilo ambalo limeanza kujengwa toka (2008) mpaka kukamilika kwake.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela anayedaiwa kuwa rafiki mkubwa wa billionea huyo alitarajiwa kuwa mmoja wa wageni maalum katika party hiyo ya siri iliyopangwa kuhudhuriwa na wageni wa VIP.

Douw Steyn
Bilionea Douw Steyn wa Afrika Kusini

Akiwa na utajiri unaokisiwa kuwa Rand bilion 8, Steyn ni mmiliki wa Hotel ya Lavish Saxon iliyoko Joburg na mwanzilishi wa makampuni ya Auto and General and Budget Insurance Company.

Kelly

Kazi na dawa! Akiwa Afrika Kusini Kelly Rowland alitweet picha akiwa anakula good time na Simba mtoto na kuelezea jinsi alivyotaka kumdhuru.

SOURCE: SOWETAN

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents