Burudani

Kevin Gates kufungwa jela miezi 30.

Rapa tokea Marekani, Kevin Jerome Gilyard, maarufu kama Kevin Gates ametupwa rumande kwa miezi 30 kwa kosa la kutishia na kumiliki silaha.

kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Gates ameshitakiwa kwa kosa hilo huku ikiwa ni Mwezi umepita, Rapa huyo mkali wa kubattle, alipmaliza kifungo chake, kwa kosa la kumpiga shabiki wake; kifungo ambacho amekitumikia kwa miezi mitano.

Gates amehamishiwa Illinois Department of Corrections, sehemu ambayo inaaminika ataweza kubadili tabia na pengine kupelekea kupunguziwa muda wa kukaa rumande. Kesi ya Gates ilitokea mwaka 2013 kwa kukutwa na silaha ya moto.

Mapema mwezi huu aliachia ngoma ya ” What If,” ambayo imetumika kwenye soundtrack ya filamu inayoongoza mauzo ya Billboard 200, ‘The Fate of the Furious’ iliyotoka mwanzoni mwa mwezi huu.

Na Laila Sued.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents