Michezo

Kibarua cha kocha Leicester City chaota nyasi

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Sky kimeeleza kuwa meneja wa klabu ya Leicester City, Craig Shakespeare ameachishwa kazi ya kukinoa kikosi hiko.

Klabu ya Leicester City imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya minane iliyocheza ligi kuu nchini Uingereza msimu huu na hivyo timu hiyo kufanya maamuzi magumu ya kuachana na kocha huyo masaa machache tu baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya West Brom hapo jana siku ya Jumatatu.

Shakespeare mwenye umri wa miaka 53, alirithi mikoba ya kocha, Claudio Ranieri ambaye aliipatia mafanikio timu hiyo kwa kuipa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu wa mwaka 2015/16.

Locha huyo ameshinda jumla ya michezo sita toka akabidhiwe timu hiyo ikiwa ni dhidi ya Liverpool ligi kuu ya Uingereza na Sevilla ambao ulikuwa klabu bingwa barani Ulaya.

Mbweha hao wa Uingereza wametumia jumla ya paundi milioni  60 kusajili wachezaji wapya ikiwa ni pamoja na ile paundi milioni 25 kwa iliyomsajili straika Kelechi Iheanacho na kiasi cha paundi milioni 15 waliyomsajili Vincent Iborra.

Pamoja na usajili wote huo imejikusanyia pointi sita pekee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents