Burudani ya Michezo Live

Kijana wa Mali aonekana shujaa Ufaransa kwa kumuokoa mtoto ghorofani, Rais amuita Ikulu (+video)

Kijana Mamoudou Gassam (22) ambaye ni raia wa nchini Mali ameonekana shujaa baada ya kumuokoa mtoto ambaye alitaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne.

Mamoudou ambaye amepata jina jipya la Spider Man, alipanda kwenye jengo hilo kutoka nchi mpaka kufikia sehemu ambayo mtoto huyo alishikilia na kufanikiwa kumuokoa akiwa salama.

Kutokana na kitendo hiko cha kijana huyo kilichookoa maisha ya mtoto mdogo, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amemualika Mamoudou Jumatatu hii kufika kwenye ikulu yake ya Elysee Palace kwa ajili ya kumshukuru zaidi.

Naye Meya wa jiji la Paris, Anne Hidalgo, amempongeza Mamoudou kupitia mtandao wa Twitter huku akithibitisha kuwa alimpigia simu kijana huyo , “Hongera kwa Mamoudou Gassama kwa kitendo chake cha ujasiri kilichookoa maisha ya mtoto jana usiku. Nilifurahi kuzungumza naye leo kwa simu, kumshukuru.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW