Burudani

Picha: Baada ya ‘Siri’ Vanessa Mdee na Barnaba wajiandaa kuachia video ya ngoma yao mpya

Ni miaka mitatu imepita tangu tulipoona Vanessa Mdee na Barnaba waliposhirikiana kufanya ngoma ya ‘Siri’ ambayo ilifanikiwa kufanya vizuri sehemu mbali mbali huku kwenye mtandao wa YouTube ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni moja.

Kwa mara nyingine tena wasanii hao wameonekana wakiwa location kuandaa video ya ngoma yao mpya.

Kwenye video ya Siri Vanessa na Barnaba walitumia location za kijiji cha Makumbusho, lakini safari hii wameonekana wakitumia mazingira ya uswahilini zaidi ambapo ni kitu cha tofauti kwa Vanessa hatujawahi kuona kwenye video zake zilizopita.

Japo haijafahamika video hiyo itatoka lini lakini kunauwezekano wimbo huo ukapewa jina la Chausiku kutokana na hashtag ambazo wamekuwa wakiweka wasanii hao kwenye picha zao walizoweka kwenye mtandao wa Instagram.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents