Michezo

Kikosi cha Julio Chakubalika

 

Wadau wasoka nchini wamewapongeza makocha wazalendo,Jamhuri Kihwelu (Julio) na Fred Felix (Minziro) kwa kuchagua kikosi cha Dar All Stars kitakachocheza na timu ya Taifa ya Zanzibar Jumapili hii.

Kikosi hicho kitacheza na Zanzibar Heroes Jumapili katika mechi maalumu ya kuwapongeza maraisi wa Tanzania na Zanzibar waliochangulia Oktoba 31 mwaka huu, huku kikiundwa na wachezaji waliokosa nafasi timu za taifa zinazojiandaa na kombe la Chalenji.

Mmoja wa wadau hao,Wema Ngumba wa Keko, Dar es salaam, aliyeshuhudia mazoezi ya timu hiyo yaliyoanza Jumatano katika uwanja wa Uhuru,alisema timu hiyo ni nzuri sana na itasaidia kujua mapungufu ya Zanzibar kabla ya kuanza kwa michuano ya Chalenji cup.

Mdau mwingine Eliah Ulaya,alisema wachezaji nyota kama Jeryson Tegete, Athumani Idd, Mussa Hassan Mgos, Ramadhani Chombo na wengineo walioachwa timu ya Taifa, ni wazuri na anaamini wataipa Zanzibar kipimo kinachostahili.

‘Makocha ndio wakupongezwa kwenye hili,kwani wao ndio wmechagua. Zanzibar Heroes wanapaswa kuichukulia mechi hiyo kama kweli ya kujipima nguvu na sio tu yakuwapongeza  marais’, alisema mdau huyo kutoka Tabata.

Mbali na mmarais, mechi hiyo vilevile inalenga kuwapongeza wabunge wote walishinda viti mkoani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents