Michezo

Kikosi cha Simba chafanya mazoezi  uwanja wa ‘Highland’ Morogoro kuelekea Kariakoo derby

 

Kikosi cha Simba SC kimeendelea na mazoezi yake  hii leo uwanja wa ‘Highland’ mkoani Morogoro kwaajili ya kujiweka sawa kabla ya kujiwinda na hasimu wake wa jadi Yanga SC mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Simba ilisafiri jana siku ya Jumapili kwenda mkoani Morogoro kwaajili ya kambi hiyo kabla hawajawavaa Yanga SC uwanja wa Taifa Aprili 29 mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa soka nchini.

Kabla ya kukutana kwa wa watani hawa wa jadi, Simba ilipoteza mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu kwa kulazimishwa sare ya bao 1 – 1 dhidi ya wenyeji wao timu ya Lipuli FC wakati kwa upande wa mabingwa watetezi Yanga  nao wakiwa ugenini hapo jana walilazimishwa sare ya 1- 1 na Mbeya City.

Msimamo wa ligi kuu Simba SC inaongoza kwa kuwa na pointi 58 dhidi ya hasimu wake yanga mwenye alama 48 akiwa nafasi ya pili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents