Michezo

Kikosi cha Simba SC kurejea jijini Dar kutokea Zanzibar

Baada hapo jana klabu ya Simba kushindwa kuendelea na michuano ya Kombe la Mapinduzi huko Visiwani Zanzibar baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa URA hatimaye timu hiyo inatarajia kurejea leo Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya msimbazi Karia Koo zi nasema kuwa kikosi cha timuhiyo kinarejea leo kutoka Visiwani Zanzibar.

Simba SC imetolewa katika mashindano ya Mapinduzi yanayoendelea huko Zanzibar ambapo kwa sasa yamefikia hatua ya nusu fainali wakati wapenzi wasoka watashuhudia Azam FC ikishuka dimbani kucheza na timu ya Singida United hapo kesho wakati Yanga SC ikicheza na URA.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents