Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Kilimanjaro Stars yatua salama Kenya na kuanza mazoezi (Picha)

Timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, iliwasili salama jana nchini Kenya tayari kwa michuano ya Cecafa 2017.

Kwa mujibu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), timu hiyo imefikia kwenye Hoteli ya Gelian na leo wamepata nafasi ya kujifua kwenye Uwanja wa Machakos Academy.

“Timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, iliwasili salama jana nchini Kenya tayari kwa michuano ya Cecafa 2017. Timu imefikia kwenye Hoteli ya Gelian na hapa wachezaji wakianza kujifua leo kwenye Uwanja wa Machakos Academy. Mazoezi yamefanyika asubuhi na jioni.” Imesema TFF.

Jumla ya mataifa tisa yanatarajiwa kushiriki michuano hiyo mikubwa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati baada ya Zimbabwe kutangaza kujitoa ambapo hapo awali kabla ya hatua hizo zilikuwa timu 10.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW