Tupo Nawe

Kinda wa miaka 24, Jordan Diakiese afariki dunia, PSG yatuma salamu za rambirambi

Mchezaji wazamani wa klabu ya Paris Saint-Germain, Jordan Diakiese amefariki jijini Paris akiwa na umri wa miaka 24.

Nyota huyo wa Ufaransa, mpaka umauti unamfika alikuwa akiitumikia klabu ya AS Furiani-Agliani ambayo ndiyo imetoa taarifa za kifo chake kupitia akaunti yake ya kijamii ya Twitter leo siku ya Ijumaa.

Mpaka sasa hakuna taarifa ya sababu ya kifo chake. Baada ya taarifa hizo klabu ya PSG imetoa salamu zake za rambirambi huku ikimuelezea kinda huyo ”Alifika katika academy za Paris Saint-Germain akiwa na umri wa miaka 13, Jordan Diakiese aliacha kumbukumbu nzuri akiwa na kocha wake pamoja na wachezaji wenzake. Nimasikitiko makubwa kwetu hii leo akiwa amefariki akiwa na umri wa miaka 24, Paris Saint-Germain inatuma salamu zake za pole kwa familia, ndugu pamoja na klabu yake.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW