Habari

Kiongozi wa upinzani DR Congo apinga matokeo ya uchaguzi, Kanisa Katoliki lamuunga mkono

Kiongozi wa upinzani nchini DR Congo, Martin Fayulu ambaye ameshika nafasi ya pili kwenye matokeo ya uchaguzi wa urais nchini humo, ameyakataa matokeo ya uchaguzi huo.

Martin Fayulu

Martin Fayulu amesema kuwa matokeo hayo yamegeuzwa, kwani yeye ndiye aliyepata kura nyingi kwa mujibu wa mawakala wake.

Matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi DR Congo, Felix Tshisekedi amepata kura milioni 7, Martin Fayulu kura milioni 6.4 na Emmanuel Shadary ambaye ni mgombea wa Serikali ya Rais Joseph Kabila ameambulia kura milioni 4.4 .

Kwa upande mwingine, Kanisa Katoliki nalo nchini humo limemuuunga mkono kiongozi huyo, kwa kusema kuwa matokeo hayo hayana uhalisia.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents