Michezo

Kisa Samatta, Haji Manara afunguka mazito ‘Ajibu matiktaka yako tunataka tuyaone Wembley au Allianz Arena’

Baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa mshambuliaji hatari wa klabu ya KRC Genk na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta kuhitajika na timu za England afisa habari wa Simba, Haji Manara amewataka wachezaji wazawa wanaoshiriki ligi kuu nchini kutobweteka na badala yake kufata nyazo za nyota huyo kwa maslahi mapana kabisa ya kwao binafsi, familia, vilabu na taifa kwa ujumla.

Afisa habari wa Simba, Haji Manara

Manara ameyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram huku akiwataja baadhi ya nyota wazawa bila kujali klabu zao wanazotumikia akiwemo Ibrahim Ajibu wa Yanga, Adam Salamba wa Simba, Mohamed Hussein na wengine.

Bao la tiktaka la  Ibrahim Ajibu wa Yanga dhidi ya Mbao FC

@official_mohamedhussein15@ibrahimajiibu23 @jonasmkude20@ndemla13 @kichuya_ @gardiel_mbaga2@feisal_salim @kev_sabato_kiduku255@yahya_zaid52 @adamsalamba na Wachezaji wengine wa kitanzania lazma muwe na jealous kwa hayo ya @samagoal77..inawezekena kabisa wengine mpo more talented kuliko yy..bt professional player ni zaid ya kipaji..ni kujitambua na kujua nn unataka..!!jiulizeni yy kaweza ana nn na nyie mshindwe mna nn ? Now tunawaimba lakini soon watawadharau..muda wa kuwa mchezaji ni mfupi..kazi yenu haifanywi milele wala haina muda mrefu..pambaneni mtoke kwa maslahi yenu,familia zenu,Vilabu vyenu na Taifa…kina Ajibu yale matiktaka tunataka tuyaone Wembley au Allianz Arena..huku utaishiwa kuandikwa na kupambwa..Sijui nimeeleweka ?au mnaniona fala !!

Samatta mwenye umri wa miaka 25, ameehusishwa kutakiwa na klabu za  West Ham United, Everton na Burnley. zinazoshiriki ligi kuu England.

Mpaka sasa nyota huyo anaeitumikia KRC Genk ya Ubelgiji ameifungia timu hiyo mabao 11 katika mechi 16 ambazo ameingia uwanjani msimu huu wakati nusu ya mabao hayo akiyafunga barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents