Kiza Kinene asema na Bongo5

1_kiza

Mkari wa ndundi ambaye inasemekana alikimbia katika usiku wa tarehe 12, pale DDC Mlimani City, Kiza Kinene ameibuka na kusema hakukimbia katika Pambano hilo ila walishindana katika masuala ya Malipo, ambayo ndiyo yaliyoleta kikwazo cha yeye kuondoka bila kupambana.


Akiongea  wa Bongo5, alisema alikuja hadi ulingoni na kuongea na mkurugenzi wa tamasha hilo Shomari Kimbau, na kuomba alipwe japo nusu ya fedha anazotaka kulipwa lakini alikataliwa na kuambiwa apande na ndipo atalipwa fedha zake, jambo ambalo hakukubaliana nalo na kuamua kuondoka zake.

Alisema kama yeye bado anahitaji pambano na Zola D, kwani hamuogopi kwake ni kama msanii wa muziki, hivyo meneja wake J.O, yupo tayari kulipa fedha za kuandaa pambano hilo kwaajiri ya yeye kupambana na Zolla D, kwani kwake bado anahitaji pambano.

1_Kiza_kinene

Shomari Kimbau:  yeye aliongea kwa kusema, aliandaa pambano  akiwa na fedha za kuwalipa, lakini mara nyingi wapambanaji unapowalipa huwa wanakimbia katika pambano na kufanya mtu kuingia hasara ya kumlipa yule aliyefika kwakuwa si kosa lake, na pia wakati yule aliyekimbia ameshachukua ‘Advance’.

Kimbau alitoa mfano katika mambo kama hayo,  Pambano la Cheka ambalo, Francess Cheka alichukuwa fedha na kutopanda kwenye pambano hadi leo hajalipa.

Pia alitolea mfano wa Mpambanaji Diksoni Mwakyembe wa Songea kwani alifika hapa kwa ajili ya pambano na sisis tumemlipia nauli, lakini akakosa mpiganaji baada ya mpizani wake kuingia mitini, na mengine mengi aliyatolea mfano.

Amesema kwa sasa wao humlipa mtu baada ya kushuka ulingoni, bila kujali anadhaminiwa na nai au amazoezi kachulia wapi wao wanachofanya ni chama cha ngumi kinasema je kuhusu hilo. basiiii.

Kiza_kinene_na_boksa

Zolla D ; kwa wakati wake naye alisema yeye hamuogopi Kiza Kinene kwani alishawahi kumpiga, ingawa anamwita mwanamuziki lakini hilo halijali anachojali ni kupata ushindi na si kingine.

Ila anamwambia anaweza kupambana naye sehemu yoyote, hata kama mitaani kwa wananchi kuzungusha duala na kuchangia yeye yupo poa, lakini alisisitiza aandae pambano kwa kufika kwenye Kampuni yake inayommiliki, ambayo ni Aurola na kisha waweke makubaliano kabla ya kwenda zake Marekani iliapande ulingoni kwaajiri ya kumaliza kazi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW