Michezo

Kizazi cha George Weah chaanza kuitikisa dunia

Mtoto wa aliyekuwa mchezaji nguli wa soka duniani, Timothy Weah amefunga mabao matatu ‘hat-trick’ na kuisaidia timu yake ya taifa ya Marekani kuchomoza na ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Paraguay katika michuano ya kombe la dunia la vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Timothy Weah anayechezea Paris St-Germain ni mtoto wa mchezaji bora wa dunia miaka ya 1995, George Weah ambaye amewahi kukipiga katika timu ya AC Milan.

Weah pia aliwahi kuchezea klabu za Monaco, Paris-St Germain, Chelsea na Manchester City katika wakati wake amewahi kutajwa kuwa mchezaji bora wa dunia mwaka 1995 na kuwa muafrika wa kwanza kutwaa tuzo hiyo.

Mtoto wa George Weah aipeleka Marekani kombe la dunia

Kwa sasa Weah ana umri wa miaka 51, na amejihusisha katika siasa ambapo kwa sasa anagombea nafasi ya Urais nchini Liberia lakini mtoto wake anajitengezea jina lake.

Meneja wa timu ya taifa ya Marekani, John Hackworth amekiambia chombo cha habari cha ESPN kuwa ni miongoni mwa vijana ambao wanajitengenezea majina yao wenyewe kama Tim na si kwa majina ya wazazi wao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents