Tupo Nawe

Klopp aitabiria Leicester kumaliza ndani ya ‘Top Four’ PL na kushiriki UEFA Champions League 

Jurgen Klopp anaamini klabu ya Leicester inayonafasi ya kumaliza nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza ikiwa chini ya aliyekuwa kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers.

Image result for Jurgen Klopp to Leicester

Leicester kwasasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League ikiwa na pointi 14 baada ya kuwa na mwanzo mzuri wa msimu huku ikishika nafasi ya pili kama itaweza kuifunga vinara Liverpool na kuizidi Manchester City ambayo ni ya pili yenye alama 16.

‘The Foxes’ ilifanya kitu ambacho hakikutarajiwa na wengi msimu wa mwaka 2015/16 baada ya kutwaa ubingwa wa Premier League mbele ya makocha bora kabisa Jurgen Klopp na Pep Guardiola na kushiriki michuano ya UEFA Champions League.

Kutokana na kuwa na mwanzo huo mzuri Klopp amesisitiza kuwa kikosi chao ni bora kwa sasa hivyo kinaweza kumaliza msimu kikiwa kwenye timu nne za juu na kushiri michuano hiyo ya Ulaya kwa mara nyingine.

“Inaonekana kama hivyo kwa asilimia 100, hawana tofauti na wale wengine waliyopo ndani ya sita bora rabda utofauti ni majina tu.” amesema Klopp.

“Ukiangalia safu yao ya ulinzi ni imara, viungo wake wabunifu, wachapakazi na washambuliaji wake wapo vizuri na hivyo ndiyo kikosi kinavyotakiwa kutengenezwa.”

Rodgers alikuwa mwenye furaha ndani ya misimu yake mitatu aliyokuwa akiifundisha Liverpool kabla ya kutimuliwa mwezi Oktoba mwaka 2015 na Klopp kurithi mikoba yake Anfield.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW