Michezo

Kocha mpya wa Simba SC kuishuhudia Singida United uwanja wa Taifa

Klabu ya Simba imedhihirisha kuwa kocha wake mpya waliyemtambulisha leo hii, Mfaransa Pierre Lechantre atashuhudia mechi ya ligi kuu soka Tanzania Bara baina ya waajari wake hao wapya dhidi ya Singida United mchezo utakao pigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kupitia mtandao wao wa kijamii wa klabu ya Simba umesema kuwa Lechantre atashuhudia mtanange huo ambao timu hiyo italazimika kuchomoza na ushindi ili kujihakikishia inakuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu.

KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA SINGIDA LEO;

  1. Aishi Manula
  2. Nicholas Gyan
  3. Eresto Nyoni
  4. Asante Kwasi
  5. Juko Mushidi
  6. Jonas Mkude
  7. Jems Kotei
  8. Mzamiru Yasin
  9. Mwinyi Kazimoto
  10. John Boco
  11. Shiza Kichuya

WACHEZAJI WA AKIBA

-Emanuel Mseja

-Said Hamis

-Mohamed Ibrahim

-Mothes Kitandu

-Emanuel Okwi

-Mohamed Husen

-Yusufu Mlipili

 

Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kwamba imempata kocha wake Mkuu mpya, Mfaransa Pierre Lechantre.
Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Afrika 2000.
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 ba pia barani Asia mwaka 2012.
Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi.

Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa

Imetolewa na
Haji Manara
Mkuu wa Habari Simba SC
Simba Nguvu Moja

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents