Tupo Nawe

Kocha wa Liverpool, Jürgen Klopp ajibu alivyojipanga kumdhibiti Messi ‘wengi wameshindwa, nitajaribu’

Kocha wa klabu ya Liverpool, Jürgen Klopp amejibu namna alivyojipanga kumkabili mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi kwenye mchezo wa nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Image result for klopp vs messi
Jurgen Klopp na Lionel Messi

Klopp akiongea na waandishi wa habari jana usiku nchini Ureno baada ya mchezo kati Liverpool na FC Porto, amesema kwanza anamshukuru Mungu kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

Kuhusu kumdhibiti Messi Klopp amesema anahitaji siku chache kuangalia namna atakavyomkabili ingawaje anajua ni kazi ngumu kumkabili.

“Namshukuru Mungu, ila sina wazo lolote kwa usiku jinsi ya kumkabili Messi. Nashukuru Mungu nitakuwa nina siku chache kama hizi za kufikiri namna ya kumzuia Messi, najua wengi wameshindwa ila nitajaribu.”.

Barcelona watavaana na Liverpool kwenye hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Mchezo wa kwanza utapigwa May 1, 2019 kunako dimba la Camp Nou na mchezo wa marudiono utapigwa May 7, 2019 Anfield.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW