Uncategorized

Guardiola alia na VAR, adai bao la Sterling halikuwa la ‘Offside’

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameonekana kutofurahishwa na maamuzi yaliyofanywa na muamuzi kupitia ‘VAR’ yaliopelekea kupewa goli mpinzani wao Tottenham huku kwa upande wao wakinyimwa bao la dakika za mwisho lililofungwa na Raheem Sterling.

Kupitia mahojiano yake na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Guardiola amesema kuwa naunga mkono mfumo huo mpya lakini katika upande mmoja na kwa upande mwingine bao la Fernando Llorente mkono ndiyo umeufuata mpira na siyo mpira umeufuata mkono.

“Na kubaliana na VAR lakini pengine kwa upande mwingine Fernando Llorente mkono uliufuata mpira (aliunawa), huwenda kwa upande aliyokuwepo mwamuzi haukuonyesha hivyo,” amesema Guardiola said.

“Naamini mpira ni huru na haki. Kama ni ofsaidi ni ofsaidi na kama sio basi iwe sio ninaimani hapo baadae na hata sasa itakuwa wa haki.”

Kwenye mchezo huo wa hapo jana Manchester City iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4 – 3 dhidi ya Tottenham hata hivyo matokeo hayo hayakuweza kuisaidia timu hiyo kusonga hatua ya nusu fainali kutokana na kufanya matokeo ya jumla kuwa na magoli 4 – 4 Spurs ikinufaika na ushindi wa 0 – 1 nyumbani kwao.

Hata hivyo City ilifanikiwa pata bao la tano lakini lilikataliwa kutokana na mwamuzi kupitia VAR kuona kuwa lilipatikana kwa njia ya Ofsaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents