Michezo

Kombe la dunia la Klabu: Sanfrecce Hiroshima ya Japan yazima matumaini ya TP Mazembe

Matumaini ya TP Mazembe kufika kwenye fainali za kombe la dunia la klabu yamezimwa jana baada ya mabingwa hao wa Afrika kufungwa mabao 3-0 na Sanfrecce Hiroshima ya Japan.

_87185831_gettyimages-501182938

Mchezo huo ulipigwa kwenye uwanja wa Yanmar wa mjini Osaka, Japan.

Magoli hayo yalifungwa na Tsukasa Shiotani, Kazuhiko Chiba na Takuma Asano.

Kikosi cha Mazembe kilikuwa kikiundwa na wachezaji wa kimataifa kutoka Ivory Coast, Mali, Zambia, Tanzania, Ghana na mchezaji mmoja tu kutoka DR Congo.

Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta nao walishindwa kutamba baada ya nafasi ya pekee walizopata kushindwa kuzitumia vyema.

Sanfrecce Hiroshima itakutana na River Plate ya Argentina kwenye nusu fainali December 16 huku Barcelona ikikutana na Guangzhou Evergrande December 17.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents