Burudani

Siipendi tena Hip Hop, imepoteza ladha – Kala Jeremiah

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Mwanza, Kala Jeremiah amesema haupendi kabisa muziki wa Hip Hop wa sasa kutokana na wasanii kushindwa kuzungumzia masuala yanayoihusu jamii.

Kala

Rapa huyo ambaye ni zao la shindano la Bongo Star Search (BSS), msimu wa kwanza 2007, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa muziki wa Hip Hop umepoteza mwelekeo.

“Kwanza kabisa siipendi Hip Hop ya sasa kwasababu imepoteza ladha na mwelekeo tofauti na ya zamani,” alisema.

“Zamani watu walikuwa wakiimba vitu bila kuficha lakini siku hizi tumekuwa tukiilainisha Hip Hop sana, jambo linaloipotezea ladha na uhalisia wake kama Hip Hop. Hiyo inanisababisha niwe nasikiliza zaidi ngoma za Hip Hop za zamani ambazo kwa kweli zinaniongezea hamasa ya kubuni vitu vipya vyenye msisimko, vinavyosikilizika na mashabiki wangu,” alisema Kala.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents