DStv Inogilee!

Kosa la kuihujumu timu ya Taifa lamuweka hatiani meneja wa Simba, TFF yamshushia rungu zito

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia Meneja wa klabu ya Simba Richard Robert kutojihusisha na Mpira wa Miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni 4.

Kufungiwa kwa Robert kumekuja baada ya kukutwa na hatia ya kuihujumu timu ya Taifa na kutotii maagizo ya Shrikisho hilo (TFF).

Richard Robert amepata hukumu hiyo kwa mujibu wa kifungu n 5(2) , kifungu cha 6(c) na (h) vya Kanuni za Maadili za TFF toleo la mwaka 2013 na adhabu ya kutotii maagizo ya TFF ni kwa mujibu wa kifungu cha 41(8) cha kanuni za ligi kuu toleo LA 2013.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW