Afya

Kuanzia kesho wakazi wa Dar kupimwa afya zao bure

Wakazi wa Dar es Salaam kuanzia kesho Jumatatu Februari 4, 2019 watapata fursa ya kupimwa na kuchunguzwa afya zao bure katika viwanja vya Mbagala Zakhem.

Image result for to test disease

Zoezi hilo litadumu kwa siku tatu, na litafanywa na timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Kairuki, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwanzilishi wa hospitali hiyo, Hubert Kairuki.

Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Arafa Juba amesema shughuli hiyo itahusisha pia upimaji wa virusi vya Ukimwi, saratani ya matiti na kifua kikuu.

Kwa kawaida kipimo cha kubaini saratani ya matiti kinagharimu kati ya Sh80,000 hadi Sh100,000 lakini watakaoonekana kuwa na dalili watafanyiwa bure, hivyo ni nafasi nzuri kwa wanawake wa Dar es Salaam,“amesema Juba .

Chanzo:https://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Wakazi-Dar-kupimwa-afya-zao-bure-/1597296-4964486-ai6nviz/index.html

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents