Afya

Kung’atwa na nyuki zaidi ya watatu kuna faida mwilini, Mtalaam adai wanafunzi watafanya vizuri darasani

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wameeleza kuwa binadamu aking’atwa na nyuki hupata faida nyingi ikiwamo kusaidia kuondoa sumu mwilini.

Related image

Hayo yamesemwa juzi na Ofisa Ufugaji Nyuki kutoka TFS, Rueben Nyambita, wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki, wilayani Kisarawe pamoja na Shule ya Sekondari Pugu ya jijini Dar es Salaam.

TFS imezungumza na wanafunzi hao kwa lengo la kuwapa elimu wanafunzi inayohusu utunzaji wa misitu, faida za uwapo wake na ufugaji nyuki katika misitu mbalimbali nchini.

Hata kama mtu ataumwa na nyuki watatu au kumi bado watasaidia kuondoa sumu na iwapo mhusika atavimba sana kuliko kawaida maana yake mwili wake utakuwa na sumu nyingi, hivyo inapokutana na sumu ya nyuki inasababisha mzio,” alisema Nyambita na kusisitiza.

Iwapo binadamu ataumwa na nyuki wengi sana kwa wakati mmoja basi ni rahisi kupata madhara kwa kuwa sumu ya nyuki itakuwa nyingi mwilini, lakini nyuki wachache haina madhara, wanafunzi na wananchi msigope kuumwa na nyuki ni sehemu ya tiba,“.

Kwa upande mwingine, Nyambita amesema yapo maziwa ya nyuki ambayo ni maalumu kwa ajili ya kulishwa malkia wa nyuki na maziwa hayo mtu akitumia huongeza akili.

Maziwa ya nyuki yana protini nyingi na kwa mwenye kuyatumia anakuwa na akili nyingi sana na kama ni mwanafunzi atakuwa anafanya vizuri kwenye masomo kwa kushika nafasi za juu,” alisema Nyambira.

Chanzo:https://www.ippmedia.com/sw/habari/%E2%80%98usiogope-kung%E2%80%99atwa-na-nyuki-wanaondoa-sumu-mwilini%E2%80%99

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents