Uncategorized

Majeraha ya Harry Kane yampa presha Pochettino, huwenda akashindwa kuumaliza msimu

Kocha Harry Kane huwenda akaukosa msimu mzima uliyosalia wa Primier League kutokana na kupata majera hapo jana kwenye mchezo wa Champions League dhidi ya Manchester City ambao waliibuka na ushindi wa mabao 1 – 0.

Mauricio Pochettino ameingiwa na hofu ya kukosekana kwa nyota wake huyo kwa msimu huu unaoelekea mwisho.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza amepata majeraha baada ya kukanyagwa kwenye kifundo cha mguu kupitia beki wa kushoto wa Man City, Fabian Delph mwanzoni mwa kipindi cha pili mchezo wa robo fainali ya Champions League.

Alipoulizwa kuhusu, Kane kama atakuwa nje kwa kipindi chote cha msimu, Mauricio Pochettino amesema “Tunahitaji kuangalia hilo kesho lakini inavyoonekana na matatizo yanayofanana.”

“Najiskia vibaya, na kukatishwa tamaa na tutakuwa kwenye wakati mgumu kwenye kipindi hiki cha mwisho wa msimu.”

“Ni imani yetu siyo tatizo kubwa lakini itachukua muda kurudi kwenye hali yake ya kawaida,”

Majeraha ya ‘ankle’ aliyopata Kane safari hii, siyo kama aliyopata dhidi ya Manchester United Januari 13 ambayo yalimuweka nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents