Michezo

Kura zamsajili Harry Kane Real Madrid

Mashabiki wa klabu ya soka ya Real Madrid wameonyesha hamu kubwa ya kumuona mshambuliaji hatari wa Tottenham Spurs, Harry Kane akivaa jezi wa timu yao badala ya Neymar wa PSG kama habari nyingi zinavyozungumzia usajili wake.

Kwa mujibu wa kura zilizopigwa kupitia gazeti la Hispania la Marca, asilimia 34 ya kura zilizopigwa na mashabiki hao zimeutaka uongozi wa timu hiyo kumsajili mshambuliaji huyo hatari wa Uingereza.

Kane ameonekana kuwa hatari zaidi katika orodha ya wafungaji hatari duniani kwa mwaka huu baada ya kufunga jumla ya magoli 56 na kuwafunika Messi, Ronaldo, Neymar, Kylian Mbappe, Robert Lewandowski na wengine.

Kwa sasa Madrid ipo katika wakati mgumu ambapo inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu nchini Hispania (La Liga) ikiwa na alama 31 huku ikizidiwa alama 14 na vinara wa ligi hiyo Barcelona.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents