Michezo

Kwa moto huu Liverpool inamfunga yoyote hata Man United – Sadio Mane

Winga hatari wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane amesema kuwa kwa uwezo uliyokuwa nao kikosi chake kwa sasa kinaweza kuifunga timu yoyote duniani pamoja na Manchester United.

Mane ameyasema hayo katika kipindi hiki ambacho timu yake ya Liverpool inaelekea katika mchezo mkubwa na wa aina yake dhidi ya Manchester United siku ya Jumamosi hii ikiwa ni  mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza.

Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5 – 0 dhidi ya FC Porto katika mchezo wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hapo jana siku ya Jumanne, Mane ambaye amefunga jumla ya mabao matano katika michezo yake ya hivi karibuni amesema kuwa timu yake ya Liverpool inaweza kuifunga timu yoyote ile duniani kwa sasa.

Natambua siyo rahisi lakini mara zote nasema tunaweza kumfunga yoyote yule katika hii dunia, ukweli nikuwa Manchester United ni moja kati ya timu bora hapa Uingereza bila shaka na dunia lakini sisi pia ni miongoni mwao.

Ni ndoto za kila mmoja wetu kucheza aina hii ya mchezo na kila mmoja anatizamia hivyo.

Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino wamefunga jumla ya mabao 11 kwa umoja wao ndani ya Liverpool katika michezo mitano ya mwisho ya ligi kuu nchini Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents