Kwa rekodi hii ya Ufaransa, Uruguay atapata tabu sana !

Timu ya taifa ya Uruguay inatarajia kukabiliana na Ufaransa mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Urusi.

Kwenye mechi hii nyota wa Les Blues, Antoine Griezmann na Lucas Hernandez watakutana na wachezaji wenzao wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Godin pamoja na Jose Gimenez wakati kwa upande wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani atakutana na Kylian Mbappe huku Luis Suarez dhidi ya Samuel Umitti kwa Barcelona.

Uruguay itaingia na wachezaji wake tegemezi akiwemo Cavani akiwa sambamba na Suarez ambaye pia anahitaji utimamu wa mwili lakini pia ikitarajia kumtumia kijana waoe Maxi Gomez, Lucas Torreira wakati Rodrigo Bentancur akiwa na kadi ya njano.

Ndani ya kikosi cha Ufaransa Matuidi ataukosa mchezo huu na nafasi yake kuchukuliwa na Ousmane Dembele,  Olivier Giroud akitarajiwa kuongoza timu hiyo kwa mara nyingine beki wakulia Benjamin Pavard, Djibril Sidibe, Corentin Tolisso, Paul Pogba na Pavard.

Ufaransa imefanikiwa kutinga fainali ya kombe la dunia mara mbili na kulichukua mwaka 1998. Wakipotez kwa Ujerumani hatua ya robo fainali mwaka 2014 na hata wakishindwa 2010 .

Uruguay ikilitwaa mara mbili mwaka 1930 na 1950. Ikitolewa hatua ya 16 bora mwaka 2014 na hata 2010.

Katika kukutana kwao Ufaransa imeipiga Uruguay mara mbili ikipoteza mchezo mmoja na kutoka sare mara saba. Kwenye michuano ya kombe la dunia imekutana mara tatu wakati ikitoka sare mbili katika kukutana huko ikiwa ni mwaka 2010 na 2002 huku ikishinda huo mmoja mwaka 1966.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW