Michezo

Kylian Mbappe atoa msaada fedha zote alizokusanya kombe la Dunia

Kylian Mbappe atoa msaada fedha zote alizokusanya kombe la Dunia

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe ameonyesha moyo wa kipekee baada ya kutoa msaada fedha zote alizopata kwenye michinuano ya kombe la dunia dola 550,000 sawa na bilioni 1.2 za Kitanzania kwa kituo kinachotoa huduma ya michezo kwa watoto wenye ulemavu.

Mbappe mwenye umri wa miaka 19 ametoa kiasi hicho cha dola za Kimarekani 550,000 ambazo zinatokana na posho pamoja na ‘bonus’ ya ushindi wa kombe la dunia mwaka huu 2018.

Mchezaji huyo amefunga jumla ya mabao manne kwenye michuano hiyo akiitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa ametoa fedha hizo kwenye kituo cha Premiers de Cordee kinacho husika na kutoa bure huduma za michezo kwa watoto wasio na uwezo wa kumudu gharama pamoja na wanamichezo watoto wenye ulemavu.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha L’Equipe kutoka nchini Ufaransa kimeeleza kuwa Mbappe hajabakiza hata kiasi kidogo cha fedha hiyo aliyopata kwenye kombe la dunia ambayo ni dola 22,500 kwa michezo iliyoshiriki timu ya Ufaransa na dola za Kimarekani 350,000 kama ‘bonus’ baada ya Les Bleus kushinda taji baada ya kuifunga Croatia jumla ya mabao 4 – 2.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents