Burudani ya Michezo Live

Lady Jaydee na Spicy wathibitisha kuwa wapenzi, waeleza walivyokutana (Exclusive Video)

Lady Jaydee na Spicy wamethibisha rasmi kuwa ni wapenzi. Kwenye mahojiano na Bongo5, wawili hao wamedai kuwa wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

“Tulikutana miezi kadhaa iliyopita na tukaanza kuzungumza, tukaanza kufahamiana zaidi na leo tuko hapa,” amesema Spicy.

“Tulikutana katika mazingira kama haya, sababu wote ni wanamuziki, kwahiyo tulikutana katika mazingira ya muziki,” amesema Lady Jaydee.

Anasema walikutana nje ya nchi.

Hata hivyo Spicy amekanusha kile kilichokuwa kikielezwa mwanzo kuwa wamefunga ndoa.

Kwa upande wa namna uhusiano wao ulivyo, Spicy amesema, “Hadi sasa mambo ni mazuri, kila mtu binafsi siku zote tuna utofauti lakini mkiziongelea mnaweza kuwa na sehemu ambayo mtakutana ambapo mnaweza kuzimaliza.”

Jaydee anafahamika kwa kuwa msiri katika masuala yake binafsi, kwanini kwenye uhusiano huu amekuwa na uwazi zaidi?

“Ni kutokana na aina ya mtu ambaye niko naye,” amejibu Jide.

“Kwasababu naye ni mtu ambaye anafanya kazi kama ya kwangu kwahiyo mwisho wa siku sio rahisi sana kusema kila kitu kinaweza kisijulikane. Lakini mambo mengine ambayo yatakuwa ni ya kwetu, si lazima kila mtu awe anafahamu. Kama watu washafahamu kwamba tuko pamoja nafikiri hiyo inatosha, zaidi ya hapo waendelee kuenjoy muziki wangu na muziki wa Spicy pia,” amesisitiza Jaydee.

Kwa upande wa mapokezi wa shemeji zake, Spicy amesema watanzania wamekuwa wakimuonesha upendo wa hali ya juu.

Together ni wimbo ambao Spicy ameuandika na kuutayarisha mwenyewe japo kwenye verse ya Jaydee alilazimika kuzitafsiri na kuziboresha kuwa za Kiswahili.

Video ya wimbo huo iliongozwa na Justin Campos na ilifanyika Zanzibar.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW