Burudani ya Michezo Live

Lamine Moro apigwa faini ya Tsh 500,000, sasa kuikosa jumla ya michezo hii

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Juni 23, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao.

Mchezaji wa Yanga SC, Lamine Moro anakosa mechi tatu (3) na faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la kumrukia mgongoni mchezaji wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto na mchezaji huyo kuanguka chini katika mechi iliyochezwa Juni 17, 2020 kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 

Pia kamati hiyo imempa adhabu mchezaji wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto kukosa mechi mbili kwa kosa la kuleta vurugu.

Kamati hiyo imeiomba Yanga SC kukaa na mchezaji wake Lamine Moro kumkumbusha kuhusiana na mchezo wa kiungwana anapokuwa kwenye majukumu yake ya kuitumikia klabu yake.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW