Michezo

LeBron James apata adhabu kali haijawai mkuta NBA

Mchezaji wa mpira wa kikapu maarufu kama ‘Basketball’, LeBron James ametolewa Uwanjani na muamuzi, Kane Fitzgerald kwamara ya kwanza ndani ya miaka 15, tangu kuanza kucheza NBA kufuatia madhambi aliyocheza wakati timu yake ya Cleveland Cavaliers ikikabiliana na Miami Heat.

James ambaye ameifungia Cleveland Cavaliers vikapu 21 katika mchezo huo wa leo , wameibuka na ushindi wa jumla ya vikapu 108-97 huku akitolewa na muamuzi huyo ndani ya Uwanja na kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo kufuatia matumizi ya nguvu aliyotumia wakati akielekea kufunga.

Mshambuliaji huyo wa Cavaliers amekutana na adhabu hiyo kwa mara ya kwanza ndani ya michezo 1,082 aliyowahi kucheza tangu kuanza kwake basketball.

Sheri za NBA zina mtaka Shabiki, Muamuzi, Mchezaji na hata Kocha atakaeongea maneno machafu au vitendo vitakavyosababisha vurugu kulazimika kutolewa nje ya Uwanja.

Kupitia chombo cha habari cha ESPN baada ya mchezo huo, James amesema

“Nimeshitushwa na maamuz yaliyofanywa na muamuzi ya kunitoa ndani ya Uwanja, nilisema niambie nilichofanya lakini aliamua kunitoa, sawa yote kwa yote tulihitaji kushinda maana ushindi ndiyo kitu muhimu zaidi kwetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents