Michezo

Liverpool yakamilisha usajili wa Christian Benteke

Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Christian Benteke Liolo mwenye umri wa miaka 24, kwa ada ya usajili wa pound milioni 32.5 akitokea Aston Villa.

Liolo-559x520

Benteke amejiunga na Liverpool kumaliza utata na ukame wa magoli katika safu ya ushambuliaji huko Anfield, baada ya kuondoka kwa Raheem Sterling aliyetimkia Manchester City mwanzoni mwa juma hili.

Benteke

Benteke aliifungia Aston Villa mabao 13 katika michezo 26 ya ligi kuu ya soka nchini England aliyocheza msimu uliopita na alikua sehemu ya kikosi kilichoifikisha kwenye hatua ya fainali ya kombe la FA The Villian kabla ya kufungwa na Arsenal katika fainali.

2AC2B8CE00000578-3171206-image-a-65_1437597129151

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents