Michezo

Logo mpya ya Simba SC yazinduliwa rasmi, Kaduguda adai Mnyama ana njaa

Simba yazindua logo mpya ya klabu hiyo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa @simbasctanzania Mwina Kaduguda hiyo ni logo ya nne kwa #simbasc

Kiongozi huyo wa #simbasc amesema katika logo hiyo Mnyama Simba anaonekana kuwa ni mwenye njaa.

“Nitowe historia fupi ya logo za klabu ya simba, nimepata bahati ya kuiona Sunderland, kwa mara ya kwanza simba ndiyo ilikuwa klabu ya kwanza kutengeneza kadi ya wanachma katika nchi, zilitengenezwa 1956.”- Kaduguda

“Logo ya kwanza ya #simbasc
yenye Simba wawili. Logo ya pili ilikuja baada ya kuibadili kutoka Sunderland kuja Simba SC tukawa na Simba mwenye kichwa sio mzima, baada ya hapo kukatokea tena mahitaji akabadilishwa akawa Simba mzima ambaye tumeenda naye mpaka hii leo ambapo tuzindua logo mpya ya Simba mwenye kichwa ana njaa, anataka kutafuna watu hasa akiwa kule kwa mkapa. ”
#Bongo5updates

IMEANDIKWA NA Hamza Fumo, Instagram @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents