Michezo

Lukaku awaadhibu mabosi wake wa zamani Old Trafford

Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku aligeuka mwiba mkali wakati alipowakabili mabosi wake wazamani timu ya Everton katika michuano ya ligi kuu nchini Uingereza.

Katika mchezo huo ambao Lukaku kwa mara ya kwanza anakutana na kikosi cha The Toffees tangu alipo sajiliwa na United kwa dau la paundi milioni 75 kwa mkataba wa miaka mitano hapo jana ameifunga timu yake hiyo ya zamani katika dakika ya 89 ya mchezo na hivyo kuisaidia timu yake kuchomoza na ushindi wa mabao 4-0.

Mabao mengine yakifungwa na Valencia dakika ya 4, Henrikh Mkhitaryan dakika ya 83 wakati Lukaku 89 na Anthony Martial akishinda kwa njia ya penati dakika ya 92 ya mchezo huo.

Kikosi Cha United kilichoingia uwanjani hapo jana ni De Gea 7; Valencia 7, Bailly 6.5, Jones 7, Young 6.5; Fellaini 6.5, Matic 8; Mata 6.5 (Herrera 77), Mkhitaryan 7 (Martial 88), Rashford 6 (Lingard 60); Lukaku 7.5.

SUBS: Smalling, Carrick, Romero, Darmian

Huku kikosi cha Everton kilichoingia uwanjani hapo jana kukabiliana na United ni Pickford 5.5; Keane 5, Jagielka 6.5, Williams 5.5; Martina 6, Schneiderlin 6, Gueye 5 (Calvert-Lewin 76), Baines 5.5; Davies 5 (Sandro 66), Sigurdsson 5; Rooney 6.5 (Mirallas 81).

SUBS: Klaassen, Besic, Stekelenburg, Holgate

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents