Promotion

Maadhimisho Ya Wiki Ya Nenda Kwa Usalama Barabarani Yanayodhaminiwa na Airtel Tanzania Yaanza Jana

· Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika mkoani Iringa viwanja vya
Samora
· Airtel yakabidhi Fulana zenye Ujumbe maalum kwaajili ya
kuhamasisha usalama barabarani

Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya
kushirikiiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha ajali
za barabarani zinapungua na kudhibitiwa.

Wiki ya nenda kwa usalama barabarani inafunguliwa kitaifa mkoani Iringa katika viwanja vya Samora kuanzia tarehe 17-22 mwezi Septemba ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MHE. DKT. EMMANUEL NCHIMBI kwa niaba ya Mh, Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wakati wa hafla maalum ya makabidhiano ya Fulana Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde, alisema “Airtel tunaona ni haki na ni sawa kuendelea kuthamini usalama barabarni na tunayo dhamira thabiti ya kuhakikisha tunaelimisha na kuhamasisha jamii na waendesha vyombo vya moto kuzingatia na kutii sheria za usalam barabarani, hivyo basi tunaomba watanzania kuunga mkono jitihada hizi ili kuhakikisha kwamba vyombo vya moto
zinakaguliwa na kubandikwa stika maalumu za nenda kwa usalama barabarani”

Airtel inadhamini kampeni hii kwa miaka 4 mfululizo ambapo mwaka huu mbali na kuchapisha stickers imejitolea fulana 800 zenye thamani ya Tsh 8 zilizo na ujumbe maalumu kwa mwaka huu usemao³ Pambana na ajali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria² makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za makao makuu ya polisi usalama barabarini jijini Dar es saalam.

“Airtel Tanzania imeamua kuunga mkono kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa sababu ya ongezeko kubwa la ajali za barabarani ambazo
zinaathiri wateja wetu, aliongeza Bi Mtinde.

Bado Airtel haitaishia hapo tayari tumeshajipanga kufanya kampeni mbalimbali zitakazokuwa zikitoa elimu kwa watumiaji wa barabara hasa waenda kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kupunguza ajali barabarani huku tukishirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani. alimaliza kwa kusema

Nae kamanda Mkuu wa Usalama Barabarani Mohamedi Mpinga alisema “Ninawashukuru sana Airtel kwa ushirikiano wenu katika mkakati wetu wa
kupunguza ajali barabarani, hadi sasa maandalizi yote ya wiki ya nenda kwa usalama yamekaa sawa na nawahamasisha sana wananchi wote wajitokeze katika vituo vyetu vyote nchini ili waweze kukagua magari yao na kujipatia stika za
usalama barabarani Kwa mkoa wa Iringa ambapo ndiko tunafanya maadhimisho ya Usalama barabarani pia tutafanyia ukaguzi pale katika viwanja vya Samora vilevile kituo cha polisi kati maeneo ya sokoni, kituo cha checkpoint ivumbilo na kile cha
mafinga, alimaliza kwa kusema Kamanda Mpinga

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents