Michezo

Madrid bingwa UEFA akimfunga Atletico Madrid leo?

Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania hii leo itaingia katika dimba la Vicente Calderon, kuwakabili mahasimu wao, klabu ya Atletico Madrid, katika michuano ya kombe la klabu bingwa barani ulaya. Madrid Derby itachezwa huku Atletico Madrid ikiwa na kumbu kumbu ya kufungwa magoli 3 kwa bila katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika dimba la Benarbeu ambapo klabu ya Real Madrid ilikuwa mwenyeji.

Klabu ya Real Madrid itaingia uwanjani wakiwa na nia ya kuwa timu ya kwanza katika michuano hiyo kuchukua kombe la Champions League mara mbili mfululizo, ilhali kwa Kocha Diego Simeone, Atletico wao hii leo watacheza kwa juhudi zote ili kuchomoza na ushindi ambao kama si kupita katika hatua ya fainali basi kuuwekea heshima uwanja wao wa Vicente Calderon ambao utakuwa ndio mchezo wao wa mwisho kuutumia uwanja huo.

Simioni, anaamini timu yake itafanya maajabu katika mchezo wa soka kama waliyofanya klabu ya Barcelona walipokutana na PSG, anaamini atachomoza na ushindi katika mchezo huo na kubadili ubao wa matokeo yaliyopita ambayo Madrid walishinda kwa magoli 3 kwa 0 na hivyo kuwapatia matumaini ya kuingia hatua ya Fainali.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents