Michezo

Man United hii moto wakuotea mbali

Mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza umemalizika baina ya Liverpool ambao walikuwa wenyeji wakiwakaribisha Manchester United pale Anfield huku timu zote zikishindwa kuliona lango la mwenzie na hivyo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

 

Mpaka sasa kikosi cha Man United kikiongozwa na Mreno, Jose Mario dos Santos Mourinho hakijafungwa hata mchezo mmoja msimuu.

Kocha machachari, Jose Mourinho ameshinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo nane akiwa kama meneja mbele ya Jurgen Klopp huku akisuluhu minne na kupoteza mitatu.

Kikosi cha Liverpool: Mignolet (7), Gomez (8), Matip (7), Lovren (7), Moreno (7), Can (7), Wijnaldum (7), Henderson (6), Coutinho (7), Salah (6), Firmino (8).

Wachezaji waakiba: Sturridge (5), Oxlade-Chamberlain (5), Solanke (5).

Kikosi cha Man Utd: De Gea (8), Young (8), Jones (7), Smalling (7), Valencia (7), Darmian (6), Herrera (6), Matic (7), Mkhitaryan (5), Martial (6), Lukaku (6).

Wachezaji waakiba: Lindelof (n/a), Lingard (5), Rashford (5).

Aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo ni Joe Gomez.

Liverpool sasa inarejea katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya huko Slovenia ikikipiga dhidi ya Maribor siku ya Jumanne kabla haijasafiri kwenda Wembley kukabiliana na Tottenham

Wakati United ikiendeleza ubabe wake wa kutokufungwa katika msimuu mpaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents