Michezo

Man United kumng’oa mchezaji tegemezi wa Aston Villa, wengine wanao waniawa sokoni hawa hapa

Manchester United inapanga uhamisho wa dau la paundi milioni 100 kumsajili kiungo wa kati wa Aston Villa mwisho wa msimu huu Jack Grealish, 24, na kinda wa Birmingham 16- Jude Bellingham. (Star)

Jack Grealish

Kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 27,anatarajiwa kuuzwa na Man United mwisho wa msimu huu . (Goal)

Winga wa Chelsea na Brazil Willian, 31, amekiri kwamba hajui pale ambapo hatma yake ipo , huku kandarasi yake ikitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu huku mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakikwama. (Evening Standard)Willianmchezaji wa Brazil na Chelsea Willian

Mkewe Willian Vanessa Martins amependekeza kwamba mumewe huenda anakaribia kukamilisha kipindi chake cha miaka saba akiichezea timu hiyo.. (Mirror)

Manchester United inaongoza ushindani wa kumsajili beki wa Borussia Monchengladbach na Switzerland Denis Zakaria, 23. (Star)

Manchester City ina matumaini kwamba mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 31, ambaye ndiye mfungaji wa mabao mengi hatawasilisha ombi la kutaka kuhamia klabu nyengine mwisho wa msimu huu , licha ya kwamba klabu hiyo huenda ikakabiliwa na marufuku ya kushiriki mechi za klabu bingwa Ulaya. (Evening Standard)Sergio AgueroJe Sergio Aguero atataka kuhamia klabu nynegine wakatia mbapo huenda Manchester City ikakabiliwa na marufuku ya kushiriki kombe la klabu bingwa ?

Barcelona inataka kumpatia kandarasi mpya kiungo wa kati wa Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 27, na wana imani kufanya hivyo licha ya kuvutia hamu kutoka timu nyengine ikiwemo Chelsea. (Sport)

Inter Milan huenda ikamnunua kipa wa Bosnia na Bournemouth Asmir Begovic, 32, ambaye kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya AC Milan, kuwa naibu wa kipa wa Slovenia Samir Handanovic, 35, msimu ujao. (La Repubblica, via Sempre Inter)

Kipa wa Real Madrid na Ubelgiji Thibaut Courtois 27, huenda asishiriki mechi nyingi na klabu hiyo msimu ujao na hata zile za kombe la klabu bingwa dhidi ya Manchester City kutokana na jeraha analouguza katika mguu wake wa kushoto. (ESPN)Thibaut CourtoisKipa wa Real Madrid Thibaut Courtois anaguzua jeraha la mguu wake wa kushoto

Leeds imejiunga na Southampton katika onyo la kutaka kumsaini beki wa Oxford na England Rob Dickie, 24. (Football Insider)

Arsenal bado inamnyatia beki wa kushoto wa Ufaransa na Paris St-German Layvin Kurzawa, 27. (France Football, via Sport Witness)

Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Ujerumani Emre Can, 26, amefichua kwamba alikataa ofa kutoka klabu tatu za ligi ya England ikiwemo Manchester United, kwa kuitii klabu yake ya zamani (Mail)

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26,Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26,

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26, alimwabia wakala wake kufutilia mbali uhamisho wake kuelekea Manchester United – wakati mwakilishi wa mchezaji huyo alipokuwa katika ofisi ya afisa mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward. (Calciomercato, via Mirror)

Real Madrid inafikiria kumsajili kipa wa Chelsea na Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, mwisho wa msimu huu, huku the Blues ikiwa na hamu ya kuwanunua makipa wawili kwa mkopo Marc-Andre Ter Stegen na mwenzake wa Manchester United na England Dean Henderson, 22. (Star)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anapanga kumpatia kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 28, mkataba mpya wa mshahara wa £350,000 kwa wiki. (Express)

  • Kevin De Bryune
Kevin De Bryune

Mlinda mlango wa England Dean Henderson, 22, amemwambia mwenzake wa Sheffield United atarudi kwa mkopo katika klabu hiyo msimu ujao iwapo hataanzishwa katika klabu ya Manchester United. (Mail)

Arsenal huenda ikamuwania mchezaji wake wa zamani wa timu ya vijana Donyell Malen aliyeondokja Arsenal na kujiunga na klabu ya PSV mwaka 2017. (Le10Sport)

Kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher, 20, aliye kwa ,mkopo katika klabu ya Swansea, ananyatiwa na klabu ya Uholanzi Vitesse Arnhem kwa usajili wa mkopo. (Sun)

Manchester United wana matumaini wanaweza kumshawishi winga wa Uholanzi Tahith Chong mwenye umri wa miaka 20 kusalia katika klabu hiyo , licha ya klabu ya Barcelona , Inter na Juventus kuoneshania naye. (Sun)Tahith ChongTahith Chong

Tottenham inafikiria kumsajili beki wa kushoto mwisho wa msimu huu na wamemlenga mchezaji anayedaiwa kuwa na thamani ya £22m Borna Barisic, 27 , raia wa Croatia ambaye kwa sasa anaichezea Rangers. (90 Min)

Kocha wa Manchester Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba Manchester United inahitaji wachezaji wawili ama watatu wapya ili kuonekana kama washindani wa taji la ligi ya Uingereza licha ya kuilaza Manchester City nyumbani na ugenini msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 10 (ESPN)

Mshambuliaji wa Ufaransa na Chelsea Olivier Giroud, 33, amefichua kwamba alizuiliwa kujiunga na Tottenham katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (90 Min)Olivier Giroud

Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud

Giroud amekiri alikuwa na hamu ya kujiunga na Inter wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari (Calciomercato)

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ambaye anaendelea kuhusishwa na uhamisho amesisitiza kuwa anafurahia kusalia Arsenal. (Mirror)

Chelsea inaongoza ushindani wa kutaka kumsajili mchezaji wa klabu ya Aldershot na England ,17, Reece Wylie. (Team Talk)

Winga wa Bournemouth na Wales Harry Wilson, 22, anayecheza kwa mkopo Liverpool , alipigwa picha akiwa amevalia koti jekundu katika mkutano huo wa klabu hizo mbili siku ya Jumamosi lakini akasisitiza kwamba alipatiwa na mfanyakazi wa Liverpool kwa sababu kulikuwa baridi.. (Liverpool Echo)Pierre-Emerick AubameyangMshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang

Liverpool huenda ikapewa fedha mwisho wa msimu huu kufuatia kifungo cha sheria cha asilimia 30 alichowekewa mchezaji wa Uhispania Luis Alberto, 27, kwenda Lazio na mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Michael Edwards. (Star)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents