Tupo Nawe

Manara ajilipua ”Kumshinda Baba lao ni Big NO, ‘Four against One”

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Sande Manara ameonekana kama vile ametupa dongo gizani, hii ni mara baada ya aliyekuwa msemaji wa Yanga, Jerry Muro kutangaza kurudi jangwani hapo jana kwenye kikao chake na waandishi wa habari.

Mapema asubuhi ya leo, Manara ameandika kuwa wanne dhidi ya mmoja, huku akiorodhesha picha ya watu wanne ambao ni kutoka kwa hasimu wao Yanga ambao ni Jerry Muro, Jimy Kindoki, Hassan Bumbuli na Antonio Nugaz.

Haji Manara ”Four against One!!! Jumlisha na kamati zao za hamasa tatu!!!, Aliyepewa kapewa tu, hata wakiungana hawa wote na wachukue na Ben Bat,,kumshinda Baba lao ni Big NO.”

Haji mwingine atazaliwa mwaka 2220 ,,kwa sasa Kuna Only one De la boss Afrika hii.” Ameongeza Manara

Hapo jana siku ya Jumanne aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro alionekana kwenye Makao Makuu ya timu hiyo iliyopo maeneo ya Jangwani na kuweka wazi kuwa amerejea licha ya kuwa hatokuwa msemaji tena lakini atatoa mchango wake kwa namna moja ama nyingine.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW