Tia Kitu. Pata Vituuz!

Manchester City hawa hapa Champions League, Real Madrid wajipange, watangaza kutumia dimba la Atletico

Manchester City watafanya mazoezi katika uwanja wa Atletico Madrid Jumatano asubuhi kabla ya mechi yao na majirani zao Real katika Bernabeu usiku huo.

City to use Wanda Metropolitano ahead of Madrid UCL clash

Pep Guardiola amechagua uwanja wa Atletico, Wanda Metropolitano kuwa sehemu ambayo wataitumia kwa mazoezi kujiandaa na mchezo wa Champions League dhidi ya Real Madrid hatua 16 mechi itakayopigwa Hispania katika dimba la Bernabeu.

Manchester City watasafiri mapaka Hispania siku ya Jumanne na kufanya mazoezi katika uwanja huo wa Atletico Jumatano kabla ya usiku wa Februari 26 kushuka kwenye dimba la Santiago Bernabeu kuwakabili miamba ya soka ya nchi hiyo Real Madrid.

Taarifa kutoka Man City zilisema, Pep Guardiola amechagua uwanja wa Atletico Madrid, Wanda Metropolitano kuwa sehemu ambayo watafanya mazoezi.

Inadaiwa Mkurugenzi wa jiji amebainisha kuwa uwanja huo wa Atletico upo kwenye ratiba ya matumizi ya ligi kuu siku hiyo ya Jumanne.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW