Manchester United mbioni kuhama Old Traford

Mkurugenzi Mkuu wa Manchester United, Richard Arnold, amesema klabu hiyo inaweza inaweza kukosa kuutumia uwanja wao huo.

Mkurugenzi huyo akiongea na South China Morning Post, amesema wataweza kuukosa uwanja huo kwa muda kutokana na kuufanyia upanuzi ambao utkuwa na uwezo wa kuchukua watu 90,000.


Mkurugenzi Mkuu wa Manchester United, Richard Arnold

Bosi huyo ameongeza pia jengo ambalo lenye nafasi ya kufanyiwa upanuzi huo ni jukwaa la Sir Bobby Charlton.

Hata hivyo Richard hajaweka wazi ni muda gani ambao ujenzi huo utaanza. Kwa sasa uwanja huo unauwezo wa kuchukua watazamaji 76,000.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW