Michezo

Maneno ya Mourinho kuelekea mechi ijayo ‘Tunachohitaji zaidi ni pointi kuliko pafomansi’

Jose Mourinho anaamini Manchester United imeanza kuimarika na kuwaimara kiakili lakini kwa muda huu kinachohitajika ni point kuliko pafomansi.

United imepoteza jumla ya pointi 18 kutoka timu ambayo inaongoza msimamo wa ligi ambayo ni Manchester City baada ya michezo yake minne iliyotoka bila ushindi.

Mourinho alianza Jumamosi iliyopita kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Southampton kisha kuibuka na droo nyingine ya 2 – 2  mbele ya Arsenal siku ya Jumatano.

”Kuna baadhi ya wachezaji wana tabia zao maalumu,” amesema Mourinho akiwa anakabiliwa na kibarua kingine dhidi ya Fulham kwenye dimba la  Old Trafford siku ya Jumamosi.

”Wacha nikupe mfano, Ander Herrera na Marcus Rashford hawa ni wachezaji wenye aina ya tabia ya pekeyao ambapo hata kama mchezo hauitaji nguvu utaona shauku yao, matamanio yao na kujitolea kwao muda wote.”

”Nilazima tujaribu kwendana na mchezo, nafahamu ni siku mbili tu nafahamu siyo rahisi. Lakini hakuna sababu, nilikuwa hapa wiki chache zilizopita nikizungumzia mwezi huu wa Desemba na hakuna kushindwa huo ndiyo ukweli, kupambana na kuwa na moyo tunahitaji ushindi.”

United inakabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi katika michezo yake ya wikiendi hii, Alexis Sanchez na Victor Lindelof wataendelea kuwa nje.

Chris Smalling, Eric Bailly, Phil Jones na Anthony Martial hawapo vizuri kiafya na wataendelea kuangaliwa hali zao hii leo siku ya Ijumaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents