Habari

Manowari ya Marekani iliyozamishwa vita ya pili ya dunia yaonekana

Mabaki ya manowari ya jeshi la Marekani USS Lexington iliyozamishwa miaka 76 iliyopita, wakati wa vita yapili ya dunia yameonekana katika sehemu ya bahari nchini Australia.

Meli hiyo imegunduliwa na meli ya utafiti wa kibinafsi ya bilionea Paul Allen, R / V Petrel ambao waliipata Lexington ikiwa chini ya maji urefu wa maili kilomita 500 kutoka pwani ya mashariki mwa Australia.


Meli ya USS Lexington wakati ilipokuwa inazama baada ya kutunguliwa na bomu

Pia zimeonekana ndege 11 za kivita kati ya 35 ambazo zilibebwa na manuari hiyo. Zaidi ya wanajeshi 200 waliuawa wakati wa kuzama kwa meli ya USS Lexington.

Hata hivyo imedaiwa kuwa meli hiyo haitaondolewa baharini kwa sababu jeshi la wanamaji la Marekani linaitaja kuwa kaburi la vita. Wakati huo huo mwaka uliopita Vulcan ilingundua mabaki ya meli ya USS Indianapolis, ambayo ilizama mwezi Julai mwaka 1945.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents