Habari

Marekani: Aliyeandika kitabu cha uhujumu uchumi, usafirishaji wa madawa ya kulevya na uhalifu ashtakiwa kwa ufisadi

Profesa wa Chuo Kikuu ambaye ameandika kitabu kuhusu usafirishaji wa madawa ya kulevya na jinsi uhalifu unavyopangwa ameshtakiwa na mamlaka za Marekani kwa kosa la uhujumu uchumi wa kiasi cha dola milioni 2.5 kutoka kwenye akaunti ya Venezuela.

Bruce Bagley

Mwendesha mashtaka anadai kuwa Bruce Bagley alipokea fedha kutoka akaunti ya benki ya Switzerland na Umoja wa Falme za Kiarabu na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 kwa ajili yake mwenyewe .

Miaka minne iliyopita, Profesa huyo aliandika kitabu kuhusu usafirishaji wa madawa ya kulevya, jinsi uhalifu unavyopangwa na vurugu zilizopo nchini Marekani, ambacho sasa kinasemwa kuwa Uhujumu uchumi ni shughuli inayokua .

Image result for Bruce Bagley

Akizungumza kupitia chombo cha habari cha CBS News, profesa wa masomo ya kimataifa katika chuo kikuu cha Miami amekanusha madai hayo dhidi yake na kusema: “Ninajihisi vizuri tu , sina hatia .Hivyo ndivyo ninavyojisikia. Wananishutumu uongo tu.”

 Mchakato mgumu

Mamlaka za New York zimedai kuwa Bagley alifungua akaunti katika benki ya Florida kwa ajili ya kampuni ambayo ilimtaja yeye na mke wake kuwa afisa na mkurugenzi.

Mwezi Novemba 2017, akaunti hiyo ilipokea ufadhili kutoka nchi za falme za kiarabu kwa ajili ya kampuni ya chakula inayoendeshwa na raia wa Colombia.

Raia wa Colombia ambaye alikuwa na akaunti ughaibuni hajabainisha ufadhili ulitumikaje vibaya huko Venezuela.Venezuela

Venezuela imekuwa kikabiliwa na changamoto za kisiasa na uchumi kwa miaka kadhaa

Kitabu cha Bagley kinaelezea namna shughuli za uhujumu uchumi zinavyofuata mlolongo mkubwa.

Mwendesha mashtaka anadai kuwa akaunti hizo zilitumika kupokea au kutoa rushwa na kutumika kwa shughuli za ufisadi nchini Venezuela.

Kesi hii ni sehemu ya jitihada ambazo Marekani wameziweka kutekeleza sheria za kuwakamata wahujumu uchumi wanaovuruga mfumo wa uchumi wa Marekani kutokana na utajiri wa mafuta nchini Venezuela.Washington

Washington

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Bwana Bagley anashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha kwa kuwa na akaunti mbili za fedha na kila kosa atahukumiwa miaka 20 gerezani.

Baada ya kufika mahakamani huko Miami, aliachiwa huru kwa dhamana ya kiasi cha dola za Marekani 300,000.

Pamoja na taaluma yake, profesa alikuwa na ushahidi mahakamani dhidi ya kesi yake kwa kuwa na mashahidi wenye taalumu walizungumza kumtetea.

Kutokana na kesi inayomkabili bwana Bagley, mkurugenzi msaidizi wa shirika la kijasusi FBI William Sweeney alisema: “Wahalifu huwa wanatumia kila mbinu za uhujumu uchumi katika uhalifu wao ili waweze kufanikiwa nia yao na kupata mwanya wa kuficha fedha zao.”

Wakili wa profesa huyo Daniel Forman aliliambia gazeti la Miami Herald kuwa amejipanga vizuri kutetea kesi hiyo na kushinda .

Chuo kikuu cha Miami kinasema kuwa Bagley yuko likizo na kueleza kuwa kesi inayomkabili ni mambo yake binafsi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents